Kwa kuwa Mungu Huona mioyo na nia za watu, hakuna kinachoweza kufichwa Kwake. Kila kitu ambacho mtu anafanya maishani kitafunuliwa mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu, na kila mmoja atahukumiwa kulingana na matendo yake. Kwa hiyo, Biblia inasema, “enendeni kwa hofu ya kumcha Mungu wakati wenu wa kukaa hapa duniani kama wageni.”
Kulingana na mafundisho ya Kristo Ahnsahnghong na Mungu Mama, Waliosema, “Lolote mlilofanya kwa mmojawapo wa hawa walio wadogo, mlinitendea Mimi,” waumini wa Kanisa la Mungu kwa unyenyekevu wanatumikiana na kuonyesha upendo. Isitoshe, wanachukua kama funzo maangamizi yaliyosababishwa na kunung’unika na kulalamika kwa Waisraeli na uasherati wa Hofni na Finehasi, wana wa kuhani, na sikuzote wanajitahidi kuishi maisha matakatifu ya imani.
Kwa maana imeandikwa: “Kuweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni mtakatifu.” Kwa sababu mnamwita Baba ahukumuye kila mtu kulingana na matendo yake pasipo upendeleo, enendeni kwa hofu ya kumcha Mungu wakati wenu wa kukaa hapa duniani kama wageni. 1 Petro 1:16–17
Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa: Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu. Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au baya. Mhubiri 12:13–14
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha